Friday, May 31, 2013

Karibu Fair 2013 inaanza rasmi leo (31st May 2013), Huko Arusha

File photo - Karibu Fair 2012
Ni Maonyesha ya kila mwaka ya sekta yaUtalii yaliyopata kujijengea heshima kubwa kwenye ukanda huu yanaanza rasmi hii leo (31st May 2013) huko Arusha. Yataendelea mpaka tarehe 2 June 2013. Maonyesho haya huweka pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii toka pande zote za nchi yetu, nchi jirani na mawakala wa utalii toka pande zote za dunia ili kuona nani anafanya nini. Maonyesho haya hufanyika kwenye viwanja vya Magereza, Nje kidogo ya jiji la Arusha karibu kabisa na uwanja mdogo wa ndege wa Arusha. Picha juu ni munoekano wa uwanja wa maoneshoya mwaka jana (2012).

Wednesday, May 29, 2013

Mkeka wa barabara ya Bagamoyo - Msata unakaribia kufika Bagamoyo

Bagamoyo Msata
Ni Barabara yenye urefu wa Kilomita zipatazo 64 yenye kuunganisha Mji wa Bagamoyo na njia kuu ya Chalinze - Segera. Barabara hii imekuwa chini ya matengenezo na hali ilivyo sasa inaridhisha kwani ni takriban kilometa 15 zimebakia ili lami iweze kufika Bagamoyo. Kamera ya TembeaTz ilipita mitaa hii tarehe 26 Mei na kushuhudia hatua kubwa waliyopiga wakandarasi hao. Kwa wale wazoefu wa barabara hii, Mkandarasi yupo karibu kabisa na kile kijiji (maarufu kwa kuuza Nyanya na Vitunguu) baada ya kuvuka daraja la Mto Ruvu.

Bagamoyo Msata
Kwa mujibu wa mwenyeji niliyeongozana nae, hivi sasa wasafiri wengi wa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro na Arusha) wamekuwa wakiitumia hii barabara kukwepa foleni na usumbufu wa unaotokana na ujenzi wa barabara ya Morogoro maeneo ya Kimara. licha ya usumbufu wa foleni, Barabara hii inaelzwa ya kuwa inampunguzia msafiri takriban kilometa zipatazo 60 kwenye safari yake kama angeendelea kwenda Chalinze, Kibaha mpaka Ubungo.

Bagamoyo Msata
Ikikamilika kabisa, ni dhahiri wasafiri wengi wa mikoa ya kaskazini watakuwa wakiitumia

Bagamoyo Msata
Kwa sisi tunaopenda mambo ya pori, basi milango ya hifadhi ya Taifa ya Saadani itakuwa imefunguliwa. Kwa kutumia njia hii, mgeni wa hifadhi ya Saadani anaweza kufika kwenye hifadhi kirahisi. Wale wanaotoa visingizio vya umbali sasa waanze kuandaa kisingizio kingine. Ni matumaini yangu pia TANAPA na wadau wengine wa utalii wanafuatilia kwa karibu ujenzi wa barabara hii na fursa ambayo itaileta kwenye hifadhi ya Saadani.

Bagamoyo Msata

Mto Ruvu kwenye njia ya Bagamoyo - Msata

Hapa ni eneo karibu kabisa na Darja la kuvuka mto Ruvu kwa yule anayetumia barabara ya Msata-Bagamoyo. 



Dara lipo ukiwa unaelekea inapoenda barabara


Ijue Blog nyingine ya Utalii Tanzania

Ni Blog ya Karibu

http://karibubongo.blogspot.com

Ungana na Mdau John Lema kwa habari mbalimbali za utalii wa hapa nyumbani Tanzania.

Karibu Fair 2013 - Maandalizi yanaendelea

Karibu fair 2013 Arusha Tanzania
Ni Picha zilizopigwa leo mchana zikionyesha maendeleo ya maandalizi ya uwanja wa maonyesho ya utalii ya Karibu kwa mwaka 2013. Maonyesho haya yataanza rasmi siku ya Ijumaa wiki hii (31st May 2013) na kufungwa rasmi siku ya Jumapili (2nd June 2013). Yanafanyika kwenye viwanja vya Magereza, nje kidogo ya jiji la Arusha karibu kabisa na uwanja mdogo wa ndege wa Arusha.

Karibu fair 2013 Arusha Tanzania

Karibu fair 2013 Arusha Tanzania

Karibu fair 2013 Arusha Tanzania
Maonyesho ya Karibu huwa ni fursa ya ajira kwa vijana mbalimbali wa jiji la Arusha na maeneo karibu. Hawa ni baadhi ya vijana waliokuwa wakisubiri nafasi zao ili waweze kupangwa kwenye maeneo mbalimbali ya shughuli za maandalizi na hatimae maonyesho yakianza rasmi.

Ulinzi umeshaimarishwa eneo la uwanja wa maonyesho



Mdau Sam Diah akiwa kwenye Zero akihakisha kuwa mambo yapo sawa

Taswira Maridhawa toka Mikumi, Game Drive ya Asubuhi

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Mikumi National Park Tanzania

Tuesday, May 28, 2013

Tembea Tanzania ipo Youtube pia

Hii ndio link ya kukufikisha kwenye channel ya Youtube ya Tembea Tanzania

http://www.youtube.com/tembeatz

Mapumziko ndani ya Zebra rock

 Zebra Rock Marangu route
Zebra rock yenyewe ikionekana kwa nyuma 

 Zebra Rock Marangu route

 Zebra Rock Marangu route
Hali ya hewa ilibadilika ikatulazimu kuvaa nguo zaidi ili kujilinda na baridi. Kwa wale wanaopenda wanaweza kuendelea mbele zaidi ya hapa na kwenda kuishia juu ya jiwe lenyewe

 Zebra Rock Marangu route
kilinge ndani ay Zebra Rock point

Ni Safari ya kuelekea Zebra rock/point tukitokea Horombo

 Ni kwenye ile siku ya acclimatisation kwa yule mpandaji anayeamua kuifanyia kituo cha Horombo huwa na fursa ya kufanya safari ya kelekea eneo lijulikanalo kama Zebra rock. Hapa kuna mwamba ambao una rangi kama ilivyo ngozi ya pundamilia. Mtundiko huu ni picha safari ya kuelekea huko tukiwa maeneo mbalimbali ya safari hii. ni safari ya masaa 3 ambayo inampeleka mpandaji mpaka usawa wa mita 4000 juu ya usawa wa bahari zikiwa ni kama mita 300 zaidi ukitokea kituo cha Horombo. Mimi Kushoto na mdau Frank kulia. Nyuma ni kilele cha Mawenzi, siku hii kulikuwa na mawingu mengi.



Kituo cha Horombo kikiwa kimemezwa na ukungu



Sunday, May 26, 2013

Maandalizi ya Karibu Fair 2013 yameanza kupamba moto huko Arusha

Maandalizi ya eneo la maonyesho ya kila mwaka ya Utalii ya Karibu yameanza kushika hatamu kwenye viwanja vya Magereza, nje kidogo ya jiji la Arusha. Maonyesho hayo ambayo yataanza rasmi tarehe 31 Mei 2013 yanatarajiwa kuwaweka pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii toka ndani na nje ya nchi kwa muda wa siku tatu. Post hii inakuletea picha kadhaa zikionyesha maandalizi ya awali ya mabanda ya maonesho yakiwa yanaendelea kwenye viwanja vya Magereza.



Msimamizi wa eneo la Maonesho Bw. Hassan (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa waratibu wa maonesho haya Bw. Sam Diah(kulia)

Acting CEO wa TATOTZ Bw Cyril (kulia) akiteta jambo na Mratibu wa Karibu Fair 2013

Wamama na wadada hawapo nyuma, nao wapo ulingoni kuweka sawa mambo kwa ajili ya maandalizi ya Karibu fair 2013. Picha zote kwa hisani ya mdau Sam Diah wa Arusha

Kituo cha Mandara, kwenye njia ya Marangu - Mlima Kilimanjaro

Saturday, May 25, 2013

Kituo cha Horombo kinavyoonekana kwa mtu anayetokea Zebra point au Kibo

Horombo

Horombo

Horombo

Horombo

Horombo

Horombo

Asubuhi Moja ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi

Ni Taswira zilizopigwa Mwezi Januari Mwishoni mwaka huu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Unapokuwa umelala ndani ya Hifadhi unakuwa na fursa ya kuweza kuanza matembezi mapema kidogo tofauti na yule aliyelala nje ya Hifadhi ambae atalazimika kusubiri hadi pale ambapo geti la hifadhi litakapofunguliwa na kumruhusu.