Wednesday, October 26, 2016

Geti la Ngorongoro

Ni Geti ambalo wengi wetu hulitumia kuingia kwenye eneo la Uhifadhi la Ngorongoro ambamo ndani ya ipo Ngorongoro crater. Ningependa nifafanue jambo moja hapa, Eneo la uhifadhi la Ngorongoro ni zaidi ya Ngorongoro Crater. Crater ni moja ya vivutio vilivyopo ndani ya eneo hili na ndio ambalo huvuta watu wengi. Ieleweke ya kwamba Oldupai Gorge, Empakaai Crater na hata Eneo zilipokutwa hatua za Mwanadamu wa kale lijulikanalo kama Laetoli nayo pia yamo ndani ya eneo la uhifadhi la Ngorongoro.

Geti hili pia huwa ni njia kwa wale wageni wanaoenda hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kutokea Arusha. Unapita hapa na kuendelea na safari kuelekea Serengeti.

Wababe wa geti la Ngorongoro Crater

Monday, August 29, 2016

Saturday, August 27, 2016

Porini anaitwa Kamba kubwa

African Python Tembea Tanzania Mikumi National Park
Ukiwa porini halafu ukasikia habari ya kwenda mahali kuiona kamba kubwa basi ujue huko muendako mtaenda kuonana na unayemwona kwenye post hii. Ni Chatu. Tulibahatika kumkuta kwenye mti karibu kabisa na Bwawa la viboko ndani ya hifadhi ya taifa Mikumi. Wenyeji wanafahamu kuwa hapo ndio kijiwe chake mida ya mchana. Kusema ukweli hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza maishani mwangu kukutana na chatu akiwa kwenye mazingira yake ya kawaida porini. mara kadhaa nimewaona kwenye maonyesho au wakiwa wamefungiwa kwenye Zoo mbalimbali nilizowahi kuzitembelea.