Wednesday, May 29, 2013

Mkeka wa barabara ya Bagamoyo - Msata unakaribia kufika Bagamoyo

Bagamoyo Msata
Ni Barabara yenye urefu wa Kilomita zipatazo 64 yenye kuunganisha Mji wa Bagamoyo na njia kuu ya Chalinze - Segera. Barabara hii imekuwa chini ya matengenezo na hali ilivyo sasa inaridhisha kwani ni takriban kilometa 15 zimebakia ili lami iweze kufika Bagamoyo. Kamera ya TembeaTz ilipita mitaa hii tarehe 26 Mei na kushuhudia hatua kubwa waliyopiga wakandarasi hao. Kwa wale wazoefu wa barabara hii, Mkandarasi yupo karibu kabisa na kile kijiji (maarufu kwa kuuza Nyanya na Vitunguu) baada ya kuvuka daraja la Mto Ruvu.

Bagamoyo Msata
Kwa mujibu wa mwenyeji niliyeongozana nae, hivi sasa wasafiri wengi wa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro na Arusha) wamekuwa wakiitumia hii barabara kukwepa foleni na usumbufu wa unaotokana na ujenzi wa barabara ya Morogoro maeneo ya Kimara. licha ya usumbufu wa foleni, Barabara hii inaelzwa ya kuwa inampunguzia msafiri takriban kilometa zipatazo 60 kwenye safari yake kama angeendelea kwenda Chalinze, Kibaha mpaka Ubungo.

Bagamoyo Msata
Ikikamilika kabisa, ni dhahiri wasafiri wengi wa mikoa ya kaskazini watakuwa wakiitumia

Bagamoyo Msata
Kwa sisi tunaopenda mambo ya pori, basi milango ya hifadhi ya Taifa ya Saadani itakuwa imefunguliwa. Kwa kutumia njia hii, mgeni wa hifadhi ya Saadani anaweza kufika kwenye hifadhi kirahisi. Wale wanaotoa visingizio vya umbali sasa waanze kuandaa kisingizio kingine. Ni matumaini yangu pia TANAPA na wadau wengine wa utalii wanafuatilia kwa karibu ujenzi wa barabara hii na fursa ambayo itaileta kwenye hifadhi ya Saadani.

Bagamoyo Msata

No comments:

Post a Comment