Tuesday, May 28, 2013

Ni Safari ya kuelekea Zebra rock/point tukitokea Horombo

 Ni kwenye ile siku ya acclimatisation kwa yule mpandaji anayeamua kuifanyia kituo cha Horombo huwa na fursa ya kufanya safari ya kelekea eneo lijulikanalo kama Zebra rock. Hapa kuna mwamba ambao una rangi kama ilivyo ngozi ya pundamilia. Mtundiko huu ni picha safari ya kuelekea huko tukiwa maeneo mbalimbali ya safari hii. ni safari ya masaa 3 ambayo inampeleka mpandaji mpaka usawa wa mita 4000 juu ya usawa wa bahari zikiwa ni kama mita 300 zaidi ukitokea kituo cha Horombo. Mimi Kushoto na mdau Frank kulia. Nyuma ni kilele cha Mawenzi, siku hii kulikuwa na mawingu mengi.No comments:

Post a Comment