Sunday, May 26, 2013

Maandalizi ya Karibu Fair 2013 yameanza kupamba moto huko Arusha

Maandalizi ya eneo la maonyesho ya kila mwaka ya Utalii ya Karibu yameanza kushika hatamu kwenye viwanja vya Magereza, nje kidogo ya jiji la Arusha. Maonyesho hayo ambayo yataanza rasmi tarehe 31 Mei 2013 yanatarajiwa kuwaweka pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii toka ndani na nje ya nchi kwa muda wa siku tatu. Post hii inakuletea picha kadhaa zikionyesha maandalizi ya awali ya mabanda ya maonesho yakiwa yanaendelea kwenye viwanja vya Magereza.Msimamizi wa eneo la Maonesho Bw. Hassan (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa waratibu wa maonesho haya Bw. Sam Diah(kulia)

Acting CEO wa TATOTZ Bw Cyril (kulia) akiteta jambo na Mratibu wa Karibu Fair 2013

Wamama na wadada hawapo nyuma, nao wapo ulingoni kuweka sawa mambo kwa ajili ya maandalizi ya Karibu fair 2013. Picha zote kwa hisani ya mdau Sam Diah wa Arusha

No comments:

Post a Comment