Tuesday, December 11, 2012

Tazara yaandaa treni maalumu ya kitalii


MAMLAKA ya Reli ya Tazara inaandaa treni maalumu ya kupeleka abiria katika hifadhi ya Selous mwisho wa mwezi huu ili kuwapa fursa abiria kubadilisha mazingira katika kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka za Krismasi na Mwaka Mpya.

Safari hiyo itakayofanyika tarehe 29 Disemba mwaka huu itawawezesha abiria mbalimbali kujionea mandhari nzuri ya hifadhi ya Selous, kufurahi pamoja na familia zao pamoja na kujifunza mambo mbalimbali katika hifadhi hiyo.

Akizungumzia safari hiyo, Meneja Masoko wa Tazara Hemed Msangi alisema kuwa wamepokea maombi mengi kutoka kwa watu mbalimbali, hivyo wameona wawapatie abiria wao kitu wanachokitaka ili kukidhi matakwa yao.

“Safari hiyo ya siku moja itaanza saa 2 asubuhi na kurudi saa 1 jioni, kwa hiyo natoa rai kwa wananchi wote kutumia nafasi hiyo ili kusherehekea sikukuu kwa namna ya pekee sana,” alisema Msangi.

Msangi aliongeza kuwa abiria watachangia huduma hiyo ambapo watu wazima watalipia Sh70,000 na watoto Sh40,000 ikijumuisha nauli, chakula na vinywaji wawapo katika safari hiyo

Chanzo: Mwananchi  
******
Picha ni kutoka ktk maktaba ya Tembea Tanzania Blog. 
Hii ilikuwa ni safari iliyoandaliwa July 2009 wakati wa Sabasaba
 Bofya HAPA na HAPA kujikumbusha picha na habari za safari ya mwaka 2009

No comments:

Post a Comment