Friday, May 14, 2010

Ni Kazi ya Twiga aka Mrefu

Ukiangalia vizuri hiyo picha juu utabainisha ya kwamba karibu miti mingi imekuwa kama imekatwa ktk level moja kwa chini. Hii haimaanishi kuwa miti yote ina umri sawa bali hiyo ni ishara tosha ya kwamba eneo hili lina twiga ambao ndio wanaifanyia 'pruning' miti hii wanapokuwa wanakula. Twiga wao hawana mpinzani ktk mfumo wa chakula porini. Chakula chao kinapatikana juu ambako hakuna mnyama mla nyasi ambae anaweza kufika na ku-share nao.

Picha juu niliipiga nikiwa ktk treni maalum ya TAZARA mwaka jana mwezi wa saba (kipindi cha Sabasaba). Ilikuwa ni treni mahususi kwa ajili ya utalii. Mnapanda pale TAZARA Station na kuelekea Stand ya Kisaki. Mkiwa njiani treni hupitia pori la akiba la Selous ambako baada ya kuingia ndani ya Hifadhi, Treni hupunguza mwendo ili kutoa nafasi kwa abiria kuona wanyama watakaoukuwepo pembezoni mwa reli. Ni nafasi nzuri pia kujionea wanyama na pori la Akiba la Selous. TAZARA huwa na hizi safari kila mwaka wakati wa kipindi cha sabasaba.

No comments:

Post a Comment