Friday, January 8, 2010

Unatembelea Selous ukiwa ndani ya treni

Mara kwa mara shirika la reli la TAZARA huandaa safari ya treni maalum ambayo hupeleka wageni ktk mbuga ya selous. Safari huwa inaanza asubuhi ktk stendi ya TAZARA kuelekea Kisaki. Juu ni Treni hiyo iliyofanya safari yake mwaka jana July.

Linesman wa uwanja wa TAZARA akipepea bendera zake kuashiria kuanza kwa safari.

Treni hupunguza mwendo inapoingia ndani ya pori la akiba la Selous ili abiria muweze kuona wanyama na mandhari vizuri.


Treni ikikatiza mitaa ndani ya pori la Selous.

Wanyama mbali mbali utawaona mkiwa njiani, pande zote mbili za reli.

Hii ndio stendi ya mwisho. Hapo ni Kisaki, nje ya pori la selous.Kisaki ipo Morogoro. Treni ikifika hapa husimama na abiria wanapata nafasi ya kushuka na kutembea hapa na pale. wakati huo treni inakuwa inageuzwa (shunting) tayari kwa safari ya kurudi Dar kupitia pori la akiba la Selous.
Safari hizi ni nafasi nzuri sana kwa familia kutoka pamoja. picha juu ni Abiria wakitembea maeneo ya stendi ya kisaki wakati treni ikiwa ktk harakati za kugeuzwa tayari kwa safari ya kurudi.
Mnapokuwa njiani mnapata msosi (sehemu ya mshiko unaolipa una-cover mlo pia). Vimiminika huwa vipo buffet kama kawa.
TAZARA huandaa safari hizi kipindi cha saba saba kila mwaka. endelea kutembelea tembeatz ili uweze kujua safari nyingine itakuwa lini. Ni safari nzuri na jitahidi usiikose mdau.

Kwa kikosi cha TembeaTz safari hii ilikuwa ni nafasi murua kwa wana-kikosi kupanda treni kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment