Thursday, August 11, 2016

Campsite namba 1 - Hifadhi ya Taifa ya Mikumi


Hili ni eneo la kufanya camping ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi. hii ni aalum kwa wale wanaokuja na vifaa vyao vya kulalia na vyakula. kuni unazoziona pembeni zinawekwa na wahifadhi kwa ajili ya kuwashia moto wa ulinzi jua likizama. wageni mnalala pembeni ya moto huo.

kibanda cha pembeni ni maalum kwa ajili ya kuandalia maakuli - Jiko. Mkija camping hapa inabidi mje na gesi yenu ya kupikia na hata mpishi wa kuwaandalia maakuli. mbebe pia na vyakula pamoja na maji ya kunywa na vinywaji vyenu mnavyopendelea.

Eneo la kuwashia moto usiku. Moto ni muhimu sana kwa nyakati za usiku kwa sababu za ulinzi. wanyama wa porini huogopa moto, na unapokuwa umewashwa unawafanya wasisogee kwa karibu. jambo la msingi mnapofanya camping ni kuhakikisha kuwa moto hauzimiki. Muhimu kuweka zamu ya kuongeza kuni ili kuendelea kuuchochea moto wenu.

Hapa nilikuja kupatembelea maana mwaka 2013 nilipata nahati ya kuja kufanya tented camping kwa mara ya kwanza na kujifunza mengi sana kwa kulala kwenye hema dogo.
gonga links za hapa chini kujiona picha za safari yetu ya Camping ya mwanzoni mwa 2013.

No comments:

Post a Comment