Sunday, January 27, 2013

Tuliwaona wanne kati ya wale watano wanaounda the BIG Five

Sharubu huyu tulimuona akiwa kwenye korongo pembezoni kabisa ya lile bwawa la Viboko. Alikuwa amedhoofu huku akiwa na majeraha baadhi ya sehemu za mwili wake. Kuonekana kwake hapo Hippo Pool kulifanya usiku uwe mrefu kwani Hippo pool ipo karibu kabisa na public Campsite namba 1 tulipoweka kambi yetu.


Gamedrive ya asubuhi na mapema ililipa baada ya kumuona huyu Chui aka wa Juu mtoto akiwa amekaa chini. ki ukweli kidogo tumopite maana alikuwa amejificha vyema kwenye hayo majani makavu hali ambayo ilimfanya asiweze kuonekana kirahisi. Baada ya muda alizama kwenye korongo liliopo mbele yake. Hawa jamaa huonekana zaidi asubuhi na mapema mida  ya jioni.


Masikio nao walikuwepo kwa sana

Nyati nao walikuwepo kwa wingi. Kwa haraka haraka utaweza kubaini kuwa kwenye hii safari tumebahatika kuwaona wanyama wanne kati ya watano wanaunda the BIG FIVE. mnyama ambae hatukumuona ni kifaru ambae hayupo hifadhi ya taifa ya Mikumi. Kikubwa kilichochangia kuwaona hawa wanyama kwa muda mfupi ni ratiba ya mizunguko ndani ya hifadhi ambapo siku ya kwanza tulifanya Late aftternoon game drive na siku iliyofuata game drive ilianza asubuhi na mapema hali iliyotuwezesha kumuona Chui akiwa anajiandaa kuingia eneo lake la maficho. mida ya asubuhi na jioni huwa ni mida ya kuweza kujionea wanyama wale adimu porini.

1 comment: