Sunday, January 27, 2013

Niliamua kujenga hema mwenyewe..


Licha ya waandaji wa safari (Lakeland Africa) kuweka wasaidizi wa kutusaidia kujenga mahema yetu, mimi niliamua kuandaa la kwangu mwenyewe ili niweze kurudi nyumbani nikiwa na maarifa zaidi. Picha juu nikiwa kwenye hatua za awali la kujenga hema nililolalia usiku kwenye Public Campsite namba 1 iliyopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Hii ilikuwa ni  jana mchana mara baada ya kufika campsite.

Zoezi likiendeleaInapofika hatua ya kukunja fito ili hema lianze kupata sura ya hema na kuweza kuwa tayari kwa matumizi, unaweza ukahitaji msaada ili kukamilisha hatua hii.

Done! Japo baada ya giza kuingia mpango wa mahema ulibadilishwa na hili hema langu likahamishiwa kwengine. Campsite namba 1 ipo karibu na lile bwawa maarufu la viboko la Mikumi. Mgeni analala kwenye hema lake, liwe dogo kama hilo au unaloliona au yale makubwa kiasi.

No comments:

Post a Comment