Tuesday, March 29, 2011

Jamaa walikuwa kwenye windo...

Ukiwa unaelewa maana ya baadhi ya mikao au mienendo ya wanyama flan flan unakuwa na nafasi ya kuona matukio adimu uwapo porini. Mdau alilikuta hili kundi la ma bwana Afya likiwa kwenye minyato hali iliyashiria mazingira ya windo

Walifanya mizunguko huku wote vichwa na mikia ikiwa imefyata tayari kwa lolote muda wowote ule

hapa wanaonekana waki Zero-in kwenye windo lao

Ghafla bin vuu windo lenyewe likabainishwa; Walikuwa wanamnyemelea bwana afya jike aliyekuwa ktk joto. Waliokuwa wakiongoza mashambulizi walikuwa ni madume toka ktk kundi moja la makapela

Waliokosa walibaki kutoa macho kama mafundi saa

Bofya hapa kujikumbusha mtundiko tangulizi uliozungumzia utata wa jinsia ya bwana afya (kimuonekano)


No comments:

Post a Comment