Kuna mdau ameomba kujua gharama za day trip (kama inavyofahamika) ya kuupanda Mlima Kilimanjaro zinakuaje.
Mtanzania na raia wa taifa lolote mwanachama wa Jumuia ya Afrika mashariki, atalipa kiingilio cha TSh 1,500 kwa siku (kwa kichwa). kwa kuwa utaratibu unalazimu mgeni kuambatana na msindikizaji, wasindikizaji gharama yao ni TSH 1,450 kwa siku (kwa guide mmoja). Siku hii tulikuwa wageni wawili (1,500x2=3,000/=) na guide mmoja 1,450 na kufanya jumla ya tsh 4,450 kwa day trip yetu. Kama inavyoonekana bei inategemea idadi ya watu na wasindikizaji watakaombatana nao na siku watakazotumia kupanda mlima.
Ukiachia gharama ambazo unalipa KINAPA moja kwa moja, kunakuwa na gharama za msindikizaji mwenyewe sambamba na vifaa utakavyohitaji kupandia mlima. Gharama ya guide in USD 20.00 kwa siku (kama TZS 30,000). Kwa day trip hutahitaji vifaa vingi sana. kutegemeana na hali ya hewa. Siku tulipopanda, kulikuwa na mvua hivyo tulilazimika kuwa na makoti ya mvua. Sikuwa na haja ya kukodi viatu maalum vya kupandia mlima (vyenye kuhifadhi joto) kwani viatu nilivyokuwa nimevaa vilitosha kwa safari ya kwenda Mandara na kurudi. Ki ukweli nilikuwa nimevaa open shoes na hazikunitatiza kwa namna yoyote ile.
Sambamba na gharama za kuingilia ktk Hifadhi, kipengele cha chakula na maji ya kunywa kipewe umuhimu ktk gharama na maandalizi. Ni lazima uwe na maji ya kunywa. usiwe na chini ya lita moja na nusu - chupa moja kubwa ya maji ya Kili itakusaidia (kwa mtu mmoja). ukiwa na zaidi sio mbaya japo unaweza ukawa na mzigo zaidi. Vyakula vizuri ni vitafunwa (bites) maana baada ya purukushani za kupanda mlima, njaa hushika hatamu kiukweli. Juice ikiwepo sio mbaya ili kurudishia nguvu (sukari ya mwili). inywe wakati wa kula, wakati wa kupanda kunywa maji kukata kiu.
huu ni mchanganuo wa baadhi ya gharama za viingilio na mambo mengine machache kwa mzawa kwenda kuupanda mlima. Ieleweke, gharama zinaweza ongezeka kutokana na mahitaji mengine. mathalan, mtu atakayetoka Dar kwenda kuupanda mlima atalazimika kuandaa mahali pa kufikia Moshi mjini au Marangu kwenyewe. Ni vyema kama unapanga safari ya kwenda kupanda mlima mpaka juu uwaachie wataalam wakuandalie mchakato mzima wa gharama za kuupanda mlima kulingana na mazingira na mahitaji yako. Kwa yule mwenye usafiri wake na atatokea Moshi/Arusha kwa usafiri binafsi, TSH 50,000 inaweza kutosha japo spea iwepo karibu.
picha juu ni nakala yangu ya risiti niliyopewa baada ya kufanya malipo kwa kutumia kadi yangu ya benki (VISA). Stay tuned for more....
No comments:
Post a Comment