Tuesday, March 29, 2011

Himo Kwenyewe

Wengi tunaosafiri kwa kutumia njia ya Arusha/Moshi (mimi nikiwa mmoja wao) huwa tunamazaoea ya kusema ya "Tulipita himo saa.... au Pale himo kulikuwa na foleni kubwa kwenye mzani.." Ilihali tulipopita ni Himo njia panda. Ukweli ni kwamba pale ambapo wanapopita wengi wa wale wanaoelekea Moshi mjini na Arusha panaitwa Himo njia panda. walioweka vibao vya kuonyesha umbali wamejitahidi kuweka jina sahihi (himo jnct) lakini wasafiri ndio huwa tunateleza bila kugundua.

Himo yenyewe ipo kilometa chache toka ilipo Himo njia panda. ni kwenye njia inayoelekea Marangu/Holili ndipo unapokutana nayo. Kwa anayetokea Mwanga/Same atakata kona kuelekea kulia wakati yule anayetokea Moshi mjini atanyoosha moja kwa moja kuelekea huko. Picha juu inaonyesha Himo yenyewe inavyoonekana ukiwa unatokea Himo njia panda


hapo unakutana na njia panda ambapo kuna njia (kushoto) itakayokupelea Marangu, Rombo na tarakea na ukinyoosha moja kwa moja unakuwa unaelekea mpaka wa Holili. haupo mbali sana na hapo

No comments:

Post a Comment