Monday, February 11, 2013

Serengeti Migration, Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro crater vyaitoa TZ kifua mbele...

Ni Katika kile kinyang'anyiro cha kupata vivutio asilia saba vyenye maajabu toka barani Afrika. Kinyang'anyiro ambacho kilirindima mwaka jana kwa wadau kupigia kura vivutio 11 vilivyokuwa vikishindanishwa. Mlima Kilimanjaro, Wanyama wanaohama wa Serengeti na Ngorongoro crater ndio yalikuwa maajabu toka Tanzania ambayo yalikuwa yameteuliwa kupigiwa kura. kwa kifupi, vivutio vyote vitatu toka Tanzania vimeweza kufanya vyema.

Taarifa ya vivutio vitatu kutoka Tanzania kuingia kwenye orodha ya vivutio 7 vya ajabu barani Afrika imewekwa wazi hii leo jioni huko mjini Arusha ambako kulikuwa na sherehe rasmi ya kuvitaja vivutio vilivyoingia kwenye orodha hii baada ya zoezi la kupiga kura kusitishwa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana. Katika hafla hiyo, Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio alikuwa mgeni rasmi. Matokeo hayo yalitangazwa na Dk, Phillip Imler ambaye ni rais wa taasisi ya Seven Natural wonders of the world.

Vivutio vingine viliweza kuingia kwenye orodha hii ni Okavango Delta, Red Sea Reef, Jangwa la Sahara na Mto Nile. Tanzania ndio nchi pekee iliyoweza kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii kwa mwaka huu. Tembea Tz blog inatoa pongezi kwa wote waliotikia wito na kupiga kura na kuiwezesha nchi yetu kutoka kifua mbele kwa kuingiza vivutio 3 kwenye orodha hii. Tunaweza pale kila mmoja akishiriki kikamilifu. Pia tunamshukuru Mdau Sam Diah wa Tanzania Travel company toka Arusha aliyekuwa kaituhabarisha mwenendo wa matukio yaliyokuwa yakiendelea ndani ya hoteli ya Mount Meru mjini Arusha hii leo.
unaweza jikumbusha zaidi kuhusu kinyang'anyiro hiki kwa kubofya hapa picha zote ni toka maktaba ya TembeaTz

No comments:

Post a Comment