Ni picha zilipigwa mchana wa leo na Mdau Thomas Aliyeoko huko hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Hili ni bwawa maarufu la viboko na mamba ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. Linajulikana kama bwawa la viboko la Retima (Retima Hippo pool). Huyo kiboko sio kwamba anapigwa mwayo, hiyo ni ishara ya hatari kwa wageni wake. Viboko huonyesha hasira na hali ya utayari kwa mapambano kwa kufungua kinywa chake na kukiacha wazi. Ukiwa na watu wanaoishi maeneo ya mito yenye viboko kama kule Rufiji, hiyo ni alama ya kukimbilia eneo la usalama zaidi. Kwa hali ilivyo kwenye bwawa hili, wageni husimama upande ambao una kingo ndefu na hivyo kuwawekwa kwenye usalama kidogo na wanyama hawa.
Bwawa la Retima likiwa limesheheni viboko wa kutosha mchana huu huko Serengeti National Park
No comments:
Post a Comment