Wednesday, February 13, 2013

Naabi Hill Gate, Serengeti NP - leo mchana





Hapa ni Naabi hill (Mlima Naabi), ni eneo ambalo ndipo kuna gate la kuingila Serengeti kwa yule anayetokea Ngorongoro au kwa yule anayetoka Serengeti Kuingia Ngorongoro. Japo mpaka wenyewe kati ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti upo mbali kidogo lakini hapa ndio geti rasmi la kulipia vibali na ukaguzi mwingine. Kwa wale wanaotokea maeneo ya mbali hutumia eneo hili kama sehemu ya kupatia mlo wao wa mchana kabla ya kuendelea na safari yao. Kuna sehemu za kukaa wageni na kuweza kula chackula walichobeba kwa raha mustarehe. Bofya hapa kuona mtundiko wa zamani kidogo wenye picha za eneo la mpakani lijulikanalo kama Golini

Jengo linaloonekana kwa mbali ndio zilipo ofisi za TANAPA mahali ambapo vibali vya kuingia Serengeti vinapotolewa au kukaguliwa wakati wa kutoka. Picha zote zimepigwa na mdau Thomas wa HSK safaris hii leo

No comments:

Post a Comment