Thursday, February 14, 2013

Ugomvi wa Mipaka na majike; Retima Hippo Pool - Serengeti NP

Serengeti National Park Tanzania
Vyanzo vikuu viwili vya ugomvi na mapigano ya wanyama (hususan Madume) ni mipaka kwa wanyama wenye hulka ya kujenga himaya pamoja na haki ya kumiliki majike. Mara nyingi ukiona wanyama wanapigana, asilimia kubwa itakuwa ni madume kwa ajili ya moja ya sababu nilizozitaja. Kwenye hii picha ni Viboko wawili wakipigana ndani ya bwawa la viboko la Retima liliopo ndani ya hifadhi ya Serengeti. Viboko ni wanyama ambao hujenga himaya zao kwenye mabwawa. kutokana na ukubwa wa bwawa na wingi wa madume makubwa, kila dume kubwa huweka himaya yake ambapo dume mwingine hatakiwi kuingia. Inapotokea dume jingine linaingia kwenye himaya ya mwenzeka, tukio hilo huchukuliwa kama tukio la uvamizi hali inayompelekea mmiliki wa eneo kupambana ili kutetea himaya yake. Akiipoteza basi ndio anakuwa pia amepoteza haki ya kukutana na majike yote yaliopo kwenye himaya hiyo na ndio unakuwa mwisho wa yeye kuendeleza uzao wake. Hii inatokana pia ya kwamba viboko 'hukutana' ndani ya maji tu. Kama dume linapoteza hati miliki ya eneo basi ni sawa na mchezaji anayeamua kutundika daluga ukutani.

No comments:

Post a Comment