Thursday, May 17, 2012

Taswira za Ngorongoro Crater

Ngorongoro Crater Tembea Tanzania
 Ni Taswira zinanzoonyesha mandhari nje ya Ngorongoro crater lakini bado ni ndani ya eneo la Ngorongoro conservation authority (NCAA). Kimsingi ndani ya eneo la NCAA kuna vivutio vingi vya utalii, mojawapo ikiwa ni ile Crater ambayo ina wanyama wa porini. Zaidi ya ngorongoro crater unakutana na Olduvai (Oldupai) Gorge sambamba na Crater nyingine ijulikanayo kama Empakaai. NCAA ni eneo kubwa ambalo lina mambo mengi ya kuvutia na kujifunza na mengi mengineyo ambayo yatakuacha mdomo wazi. Mtundiko huu unakupa picha kadhaa ambazo zimepigwa ndani ya eneo la NCAA lakini ni nje ya ile crater iliyozoeleka na wengi - Ngorongoro crater. Barabara unayoiona kwenye picha ya juu ni barabara ambayo inatokea Arusha na kuelekea Hifadhi ya Serengeti mpaka maeneo mengine ya mkoa wa Mara. Ngorongoro crater ipo upande wa kulia wa hiyo barabara. Geti la kushukia crater lipo mbele kidogo ya hapo, upande wa kulia

Ngorongoro Crater Tembea Tanzania
 Niliwahi kudokoze hapo awali ya kwamba NCAA ni eneo pekee duniani ambako uhifadhi unaoruhusu shughuli za watu kuendelea ndani ya eneo la hifadhi kufanyika. Vibanda unavyoviona ni boma za wamasai ambao wao wanaishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Hakuna mahali ambapo uhifadhi wa namna hii unafanywa. Mara zote, eneo likitengwa kwa shughuli za uhifadhi basi wananchi wote wanaoishi ndani ya mipaka ya eneo huondolewa ili shughuli na taratibu za uhifadhi ziweze kuendelea. Wengi wa wananchi wanaoishi huku ni watu wa kabila la wamasai ambao wanaishi na mifugo yao sambamba na wanyama pori. Ukitembelea Ngorongoro crater usijekustaajabu kwa kuona vijana wa kimasai wakiingia ndani ya crater au wakiwa ndani ya crater na mifugo yao. Wanaruhusiwa kuingia nayo na hufanya hivyo kwa lengo la kufuata maji kwa ajili ya mifugo yao na hata malisho ya mifugo.

Ngorongoro Crater Tembea Tanzania
 Pembezoni mwa ngorongoro crater kuna milima kadhaa. Kwa yule atakayekuwa anatoka Arusha kwa gari kuelekea Ngorongoro crater atathibitisha ya kuwa safari hii hutawali na hali ya kupanda mlima. hususan kuanzia maeneo ya Karatu na baada ya kuingia rasmi ndani ya Eneo la NCAA - baada ya kupita geti la Lodware. Picha juu ni baadhi ya Milima ambayo ipo ndani ya eneo la NCAA - nje ya ngorongoro crater.

Ngorongoro Crater Tembea Tanzania
Eneo tambarare unaloliona kwa mbali ni uwanda wa Serengeti.

Ngorongoro Crater Tembea Tanzania
Picha hizi zote ni kutoka maktaba ya TembeaTz, zilipigwa mwaka 2009
Tembelea tovuti ya NCAA kwa habari zaidi ili uweze kujielimisha zaidi
http://www.ngorongorocrater.org/ 

No comments:

Post a Comment