Naibu Waziri
wa Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa (watatu kushoto) pamoja na
Mkurugenzi Mwendeshaji Biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bibi Elizabeth
Thabethe (wa kwanza kushoto) katika
picha ya pamoja na baadhi ya waoneshaji kutoka Tanzania wakiongozwa na
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki (wan ne
kushoto) alipotembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA mjini Durban
Afrika Kusini.
Geofrey Tengeneza, Durban.
Banda
la Tanzania katika maonyesho ya Utalii ya Kimataifa ya INDABA yanayoendelea
jijini Durban Afrika Kusini limeendelea kuvutia viongozi na watu wa kada
mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini wanaotembelea maonyesho
hayo. Miongoni mwa waliotembelea banda
hilo shindwa kuzuia hisia zao hususan kwa maelezo na vielelezo vinavyoonesha
uzuri na upekee wa vivutio vya utalii
vya Tanzania na shughuli za utalii zinavyoendeshwa nchini ni Naibu Waziri wa
Utalii wa Afrika Kusini Bibi Tokozile Xasa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Viwanda
na Biashara la Afrika Kusini Bibi Elizabeth Thabethe ambao kwa pamoja walitembelea Banda la
Tanzania na kujionea vielelezo mbalimbali sambamba na kupata maelezo yaliyowafurahisha
sana kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza
na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk Aloyce Nzuki na
waoneshaji wa Tanzania kwa ujumla Naibu
huyo waziri alifurahishwa na kuvutiwa na jinsi Tanzania kupitia Bodi ya Utalii
ilivyojipanga katika kuitangaza Tanzania duniani na jinsi ambavyo Tanzania imekuwa ni mshiriki
mzuri wa maonesho ya INDABA na kukiri kuwa Tanzania imekuwa ikitoa changamoto kubwa
kwa nchi nyingine wanachama wa SADC katika sekta ya Utalii. “Tanzania ni nchi
tishio katika sekta ya utalii miongoni mwa nchi za SADC, ni nchi inayonivutia
sana “ alisema Bibi Tokozile Xasa
Jumla
ya makampuni 49 kutoka sekta binafsi na taasisi sita za serikali zinashiriki
katika maonesho hayo ambayo ni makubwa kuliko yote barani Afrika. Maonesho haya
hufanyika kila mwaka jijini Durban Afrika Kusini. Katika maonesho kama haya
mwaka jana Banda laTanzania lilitunukiwa tuzo ya kuwa Banda Bora kuliko yote
katika maonesho hayo miongoni mwa nchi za SADC.
No comments:
Post a Comment