Hali ya hewa ni moja ya vitu ambavyo hupelekea watu kusafiri toka eneo moja kwenda jingine kwa lengo la kukwepa hali flani au kuifuata hali ya hewa ya namna fulani. Kwa nchi nyingi za magharibi, watu wengi hupenda kusafiri mbali na wanapoishi ifikiapo kipindi cha majira ya joto. na baadhi yao hufanya hivyo kipindi cha baridi kali. Hali ya hewa ni kipengele muhimu kukifahamu unapopanga safari yako kwenda eneo flani hususan safari ya mapumziko. hali ya hewa inaweza kukulazimisha kutofanya shughuli ambazo ungependelea. mathalan, eneo linapokuwa lipo ktk kipindi cha mvua, shughuli zinazohusisha matembezi zinakuwa ngumu kuzifanya. ufikapo msimu wa baridi, maeneo mengine huwa na baridi kali kiasi cha kufanya maisha kuwa kero badala ya mapumziko kwa wewe usiyeizoea hali ya pale.
Kwa hapa Tanzania, maeneo ya nyanda za juu kusini yanafahamika kwa kuwa na baridi kali. hali iliyopeleka mpaka wajanja kuliita baridi 'Mufindi' - moja ya maeneo yaliyopo nyanda hizo. Hivi majuzi nikiwa njiani kurudi dar mida ya asubuhi tulipita maeneo ya Njombe na makambako tukitokea mkoani Ruvuma. Mtundiko huu una baadhi ya picha nilizobahatika kupiga tukiwa njiani maeneo ya Njombe hadi Makambako ambapo tulikutana na ukungu mzito. Kuna sehemu ukungu ulikuwa ni mwingi kiasi cha kutulazimisha kupunguza mwendo kasi kwa kiasi kikubwa na kuwasha indicator za hazard kuepusha maafa ya namna yoyote ile.picha ya kwanza na ya pili ni maeneo kabla ya kufika Njombe Mjini ukiwa unatokea Songea.
Hapa ni eneo la mashamba ya chai lililopo kati ya Njombe na Makambako.
Wajenga nchi wakielekea maeneo yao ya kuwajibika. Unauona sio moshi bali ni ukungu ulitawala eneo hili.
Ukungu umetawala kila upande. Kwa mujibu wa wenyeji wetu maeneo haya sasa ndio yanaanza kuingia katika kipindi chake cha baridi japo kwa sasa haijakolea sana. Tulielezwa kuwa ifikapo mwezi Juni baridi ndio huchanganya zaidi. kwa sisi toka pwani hata hii baridi tangulizi ilitupa shida kinamna kwenda nayo sambamba, hususan mida baada ya jua kuzama. Kwa yule ambae atapenda kwenda kujipima nguvu na baridi la huko, ajipange kwenda kudhuru maeneo hayo ifikapo mwezi Juni
No comments:
Post a Comment