Hii ndio raha ya kufanya safari ndani ya pori la akiba ambako off-road driving inaruhusiwa. Baada ya kuona ishara za majani na alama za matairi ya waliotutangulia tulijikuta tukiachana na barabara na kuchoma ndani ya pori ili nasi tujaribu bahati zetu. Gari ya mbele ilikuwa ni ya wageni wengine ambao kama sie nao walikuwa na kiu ya kuwaona mchakamchaka wakiwa porini.
Njia unazoziona ardhini ni mapito ya wanyama na sio wanadamu. Hapo ni ndani ya pori kabisa. Ukiachana na barabara maalum huku cha muhimu ni umaradufu wa gari na umakini wa dereva. maana hapo njia mnatengeneza wenyewe. Kikubwa ni kufuata matairi ya wale waliowatangulia ili uweze kufika walipofika au utoke kule ulipokwenda. Navigation ndani ya mapori ya akiba na hifadhi yanahitaji zaidi ya GPS. Siku hii haikuwa bahati yetu kuwaona mbwa mwitu hao (mchakamchaka) japo baadae tulikuja ambiwa hawakuwa mbali na mahali tulipogeuzia na kurudi barabarani. Ndio vijimambo vya porini hivi...
Selous ndio pori/eneo la uhifadhi lenye mbwa mwitu ambao wapo huru wakiishi maisha ya porini. Serikali ikishirikiana na taasisi kadhaa za uhifadhi zipo mbioni kuwarudisha mbwa mwitu ktk maisha ya porini ktk hifadhi za Serengeti na kule Mkomazi. Sasa hivi mbwa hawa wanatunzwa ktk maeneo maalum ili wazaliane kabla hawajaachiwa porini.

No comments:
Post a Comment