Saturday, November 5, 2011

Ni alama kwa wengine.....

uwepo wa tawi/jani kwenye barabara na matairi yalikwenda hovyo hovyo huwa ni ishara ambazo wazee wa pori hutumia ili kupeana habari njema. mnapokuwa porini na kukutana na moja ua vitu hivi viwili sharti msimame na mgawane maeneo ya kukagua vyema. lazima hapo kuna kitu kilikuwepo au bado kipo. Sio jambo ka kupotezea.

Kulikuwa na tawi jingine upande mwingine wa barabara ili kuashiria ni upande upi wa barabara ndio kuna habari njema za kufuatiliwa. Matairi yalikwenda hovyo hovyo nayo ni kiashiria kingine kudhihirisha kwamba walitutangulia waliacha njia ya kawaida na kufuatilia. Hivi ni alama ambazo dereva au hata mgeni anaweza ziona na kuwezesha wageni kuona vitu vizuri ndani ya pori au hifadhi. ni vizuri ukizielewa hizi alama 'za porini' ili kuongeza nafasi ya kujionea vitu adimu.
Purukushani yote hii ilitokana na uwepo wa kundi la mbwa mwitu eneo hili. Wageni waliotutangulia dakika kadhaa walifanikiwa kuwaona kirahisi kwani awali walikuwa pembezoni mwa barabara kabisa. Baadae walitokomea ndani ya msitu - mbali na barabara ambako baadhi ya madereva waliwafuata.

Wazee wa pori wamewapa mbwa mwitu jina la mchaka mchaka kutokana na tabia yao ya kuwa kwenye mwendo wa mchaka mchaka muda mwingi wa siku. katika wanyama ambao hawatabiriki kuonana na wala hawakimbiliwi ni mbwa mwitu. daima wao wanakula tizi - mchaka mchaka. Ukifanikiwa kuonana nao jua hiyo ilikuwa ni siku yako.

No comments:

Post a Comment