Tuesday, October 26, 2010

Bwawa la Ranzi; Same - Mbaga

Wapo wanaloliita ni Ziwa na wengine nimewasikia wakisema Ranzi ni Bwawa. Tembeatz (kwa sasa) inalichukulia kama ni bwawa. Ni Bwawa ambalo linapatikana ktk milima iliyopo ndani ya Wilaya ya Same eneo lijulikanalo kama Mbaga. Bwawa hili lipo maeneo karibu na moja ya shule maarufu iliyopo huko milimani ijulikanayo kama shule ya Manka.

Wengi huja hapa kupumzika wanapokuwa huko milimani kwa shughuli mbali mbali. Siku hii, kikundi cha wanafunzi waliokuwa huko ktk milima ya Same kwa utafiti walitembelea eneo hili ikiwa ni sehemu ya mapumziko baada ya kazi. Walikuwa ni wageni wa moja Tona Lodge ambayo imejikita ktk utalii asilia (Cultural tourism)

Pembezoni mwa bwawa hili kuna fukwe yenye kutoa fursa ya michezo mbalimbali.


Mdau Elly Kimbwereze (Tatu skushoto) akipozi na wageni wake hao baada ya shughuli mbali mbali ktk bwawa la Ranzi. Kimbwereza ni mdau aliyejikita ktk sekta ya utalii asilia kupitia Tona Lodge iliyoko huko Mbaga.

No comments:

Post a Comment