Tuesday, July 20, 2010

Wageni wa Tona Lodge - Mbaga, Same.

Tona Lodge ni lodge ambayo imejikita ktk sekta ya utalii asilia (Cultural tourism). Hupokea wageni wengi toka nchi mbalimbali ambao hupenda kukaa vijijini na kujifunza jinsi wananchi wa vijijini hapa kwetu wanavyoishi na kuendesha maisha yao. Picha hizi ni vikundi viwili vya wanafunzi wa vyuo vikuu toka Marekani na Uingereza waliowahi ishi Tona Lodge kwa vipindi kadhaa mwaka jana.

Wanafunzi toka Yale University. hawa wao walikuja kula bata

Licha ya kuja kupumzika, kundi hili lilikuwa na wanafunzi ambao walikuwa wanafanya utafiti wa vipepeo wanaopatikana ktk milima ya pare ya kusini. Jamaa hawa waliweza kubaini species kadhaa za vipepeo adimu walio ktk milima hiyo.

1 comment:

  1. Good for Pare Mountains..they are now opened for the world to see.
    A challenge to Mbaga people to be more creative and use the opportunity wisely..

    Says..Richard Mbaga

    ReplyDelete