Sunday, July 11, 2010

Vantage Point

Ili kuweza kuiona hatari kabla haijakuwa soo, wanyama wanaoishi maeneo ambayo kuna nyasi ndefu hupenda kusimama kwenye vichuguu ili kuweza kuangalia kama kuna hatari au la. Hii inamsaidia mnyama kumuona adui yake mapema (kama yupo) hali ambayo inampa muda wa kufanya maamuzi ya nini kufanya. Picha juu ni swala tuliyemkuta karibu kabisa na geti kuu la hifadhi ya taifa ya Tarangire.

wa chini na hata wa juu wamekuwa na tabia ya kutumia magari ya wageni kama vantage point. zipo baadhi ya picha ambazo utaona chui yupo juu ya gari la wageni. Hii nayo ni muendelezo wa tabia hii ya kutumia sehemu zilizoinuka (magari) ili kuweza kuona mbali. kwa wa juu au wa chini, kupanda juu ya gari kunampa nafasi ya kuona wapi aelekee ambapo atapata mlo au wapi asipite ili asikutane na sharubu au bwana afya. Siku ukiwa porini na wa juu/wa chini akapanda juu ya gari lako jitahidi uwe mtulivu ili usimshtue. Ni nafasi za nadra sana.

No comments:

Post a Comment