Mdau, fahamu ya kwamba ndani ya hizi hifadhi zetu kuna Watanzania wenzetu ambao wamepewa jukumu la kuzisimamia hifadhi hizi wanaendelea na maisha yao ya kila siku kama kawa. Tulimkuta mama huyu akitembea bila ya wasiwasi ndani ya eneo ambalo wanaishi wafanyakazi wa TANAPA ktk hifadhi ya taifa ya Tarangire. Sehemu hii ipo ndani ya hifadhi na ki ukweli hilo ni eneo ambalo wanyama pori wapo.
Ni Shule ya msingia ambyo ipo pembeni kidogo ya eneo la makazi. Ipo ndani kabisa ya hifadhi na ni eneo ambalo wanyama wapo. Kwa mbali ni watoto wakiendelea na michezo yao kama ilivyo ada baada ya muda wa masomo kuisha. Sipati picha ya hali inakuaje kwa kusoma ktk shule ambayo uwanja wake wa michezo upo ndani ya eneo la hifadhi. Nikipata nauli, nitajaribu kufanya mahojiano na watoto wanaosoma ktk mazingira haya na changamoto wanazokumbana nazo. Siku hii ratiba haikuruhusu. Kwa ujasiri na hali hii, ndugu zetu hawa sambamba na familia zao wanastahili pongezi kwa kulitumikia taifa ktk mazingira haya
No comments:
Post a Comment