Sunday, July 18, 2010

Serengeti Na Ngorongoro crater ngoma droo

Nyumbu wakifanya safari yao ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Muonekano wa Ngorongoro crater toka Crater view point

Hifadhi za Taifa za Ngorongoro crater na Serengeti zimeibuka kidedea huku zote zikinyakua point za juu sawa kwa sawa ktk kura ya maoni iliyokuwa ikiendeshwa kupitia blog ya TembeaTz. Kura hii ambayo ilibeba swali lisemalo "Ungependa kutembeklea Hifadhi/mbuga ipi iliyopo Tanzania?" Serengeti na Ngorongoro ziliongoza mtanange huu kwa kupata kura sawa huku zikifuatiwa na pori la akiba la Selous mwishoni zikiwa ni hifadhi ya Mikumi na Tarangire nazo zote zikitoka ulingoni kwa pointi sare.

Matokea haya ni kiashiria cha ni hifadhi ipi ya hapa Tanzania ambayo wadau wa TembeaTz wanapendelea kwenda kutembelea. Mtanange huu ambao ulirindima kwa siku takriban 7 uliwapa nafasi wageni na wenyeji wa blog ya TembeaTz kuchagua hifadhi ambayo wangependa kuitembelea kama wakipata nafasi ya kufanya hivyo. Timu ya TembeaTz inawashukuru wote wale walioshiriki ktk kura hiyo ya maoni. Taarifa hizi zimetoa mwanga kwa waandaji wa safari mahususi kwa ajili ya wazalendo kujua ni wapi wazalendo wangependa kwenda kutembea na kupumzisha akili zao.

Stei tyuned kwa raund nyingine ya kura ya maoni inayuhusu maswala yetu haya...

---------------------
Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwaomba radhi wadau kwa kutoweza kwenda sambamba na mahitaji yenu ya habari kwa siku kadhaa zilizopita. Sasa hivi mambo mswano na tunapatikana hewani kama kawa. Samahani kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na hali hiyo.

1 comment: