Sunday, July 18, 2010

Maporomoko ya mto Sere; KINAPA

Ni moja ya maporomoko ya maji ya mto nilioambiwa unajulikana kama mto Sere. ni mto ambao unaanzia ktk Mlima Kilimanjaro na kupita ndani ya hifadhi ya KINAPA. Haya maporomoko tuliyafikia tukitokea maeneo karibu na geti la umbwe.

Ni eneo lenye mandhari mwanana.

Bwawa lililotengenezwa baada ya maporomoko ya maji. Kina ni kifupi, hapo unavua viatu na kuingia na kutembea bila wasi. Eneo hili lipo chini ya miti mirefu ambayo Mbega weupe (White colobus Monkeys) wanapatikana. Siku hii walikuwa mbali ndani ya msitu, tuliishia kusikia kelele zao na kuona matawi ya miti ikipepea wakati wakikimbizana.

Mandhari ya maporomoko haya ukiwa unakaribia kuyafikia. hapa ni safari ya miguu tu, gari halifiki

No comments:

Post a Comment