Sunday, July 4, 2010

Ngorongoro Crater

Moja ya mambo ambayo yanafanya eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuwa la kipekee ni uwepo wa makazi ya wanadamu ndani ya eneo la hifadhi wakiishi bega kwa bega na wanyama pori. Inaelezwa ya kwamba aina hii ya uhifadhi inatumika sehemu chache sana Africa na kwa Tanzania inatumika na Ngorongoro Conservation Area Authority(NCAA). Ndio maana ukiwa unakaribia geti la kuingia shimoni (crater) utakutana na Maasai boma ambayo ipo upande wa kushoto (ukiwa unatokea Arusha) wa barabara boma ambalo ni makazi ya familia ya kimaasai. Hapo kuna Familia za Wamaasai wakiendelea na shughuli zao za kila siku ikiwemo kuwakaribisha watalii wanaotembelea boma lao. Boma hili lipo nje ya shimo (crater) lakini ndani ya eneo la NCAA.

Ukiwa unatoka Ngorongoro kuelekea Serengeti (kwa gari) usishangae ukiona Ng'ombe wa wamasai wakiwa wanachungwa sambamba kabisa na makundi ya Nyumbu na Pundamilia ktk eneo moja. Kipindi cha kiangazi wamasai hushusha ng'ombe wao ndani ya crater ili kuweza kupata maji ambayo huwa yanapatikana kirahisi ndani ya crater kipindi cha kiangazi. (picha - TTB)

1 comment:

  1. Mara ya kwanza kuona picha ya Watalii wakiwa kwenye boma hili la Wamasai, nilishindwa kupata 'orientation' ya mahali. Leo nieweza kupanua uelewa wa jiografia ya lilipo boma na shughuli zinazotendeka humo.
    Shukrani nyingi sana KK.

    ReplyDelete