Saturday, July 3, 2010

Paa la chelewa

kila kinachopatikana katika mti wa mnazi kina matumizi yake kwa namna moja au nyingine. wengi tumezoea kuona makuti ya mnazi yakitumika kuezekea. Lakini nilipotembelea Kibosho resort hivi karibuni nilistaajabu baada ya kuona ya kuwa hata zile chelewa zinazotoka ktk kuti la mnazi na zenyewe ni nyenzo inayoweza kuezekea nyumba. Kwa wengi wetu kazi kubwa ya chelewa ni kwenye ufagio. Kwa sie tuliopitia shule za Halmashauri tulibeba sana fagio za chelewa kwa ajili ya kufanyia usafi eneo lako shuleni.

hili ni paa la moja ya bandas ktk Kibosho resort huko kibosho likiwa ktk hatua za mwisho za kuezekwa.

1 comment: