Tuesday, July 6, 2010

Maoni yako yana thamani kubwa....


Mdau,

Ikiwa ni ktk jitahada za kuvumbua namna na mbinu zitakazowezesha kuamsha mwamko kwa wazalendo kutembelea hifadhi na vivutio vinavyopatikana hapa Tanzania, blog yenu ya TembeaTz imeanzisha utaratibu wa kuweza kupata maoni toka kwenu wadau ktk kufanikisha mpango huu. TembeaTz imeanzisha kura ya maoni (Opinion Poll) ambayo ni mwanzo wa mchakato wa kuweza kubaini mahitaji ya Wazalendo ili kuwawezesha wahusika ktk kuandaa safari (Tour operators) wawe na taarifa muhimu ili kufanikisha lengo kikamilifu.
Ukiwa kama mdau wa blog ya TembeaTz na Utalii wa ndani, Unaombwa kushiriki ktk kura ya maoni kwa kuchagua jibu linalokupendezea katika mchakato unaoendelea kwenye blog ya TembeaTz. Kura hii ya maoni ipo upande wa kulia wa blog, pembezoni mwa mitundiko ya kila siku. Kama utakuwa na maoni zaidi usisite kuyatuma kwa barua pepe kupitia
tembeatz@gmail.com.

Tunawashukuru sana wale wote ambao wamekuwa bega kwa bega na TembeaTz toka ilipoanzishwa mpaka hii leo. Tunajali na kuthamini muda na jitihada zenu kwa ajili ya kuifikisha TembeaTz hapa ilipo sasa. AHSANTENI SANA na tunaomba ushirikiano wenu zaidi ili tuzidi kusonga mbele zaidi na zaidi.

KK,
Mdau mwandamizi - tembeatz.blogspot.com

3 comments:

  1. ur the best post more pictures please! St louis,usa.thanks

    ReplyDelete
  2. Blog yako huwa inaburudisha akili yangu kila ninapoifungua. Mbali na hilo kila nikiitembelea tembeatz nakuwa na uhakika wa kijifunza jambo jipya ambalo ki ukweli awali sikuwa nikilijua. keep it up Mdau.

    nimekuunga mkono mdau kwa kutoa maoni kwenye Opinion poll inayoendelea sasa.

    Tuko pamoja

    ReplyDelete
  3. TUKO PAMOJA KAKA, HII BLOG UNAIENDESHA KWA GHALAMA KUBWA SANA KUTOKUITEMBELEA BINAFSI NAJIHISI KAMA MFUJAJI

    ReplyDelete