Friday, July 16, 2010

mapambano dhidi ya ujangili

Ni jitihada za wahifadhi kuhakikisha kuwa nyara za wanyama ambazo zina thamani kubwa haziingi sokini kupitia njia za panya. Picha juu inaonyesha ngozi za pundamilia ambalo tulielezwa ya kuwa wanakuwa wamekufa ktk hali ya kawaida. Ikitokea mnyama ambae sehemu ya mwili wake ni dili mtaani, wahifadhi huchukua ile sehemu (Ngozi au Pembe) na kwenda kuihifadhi ili isiingie mikononi mwa majangili kwa kuokotwa. Unazoziona ktk picha juu ni ngozi za pundamilia ambazo zimewekwa karibu na ofisi ya TANAPA ktk hifadhi ya taifa ya Tarangire.

No comments:

Post a Comment