Tuesday, July 6, 2010

Usilolijua kuhusu Ngiri mtoto...

Ngiri watoto wanapozaliwa hutegemea Maziwa ya mama yao ili kuweza kupata virutubisho wanavyohitaji ktk ukuaji wao. Maziwa wayapatayo toka kwa mama yao ndio huwa chakula pekee watakachokitumia hadi wafikiapo umri wa takribani wiki 6 ndio nao wataachana na utegemezi wa maziwa ya mama na kuanza kula nyasi. Ktk kipindi ambacho ngiri hawali nyasi, Ngiri watoto wanakuwa na tabia ambayo kwa sisi binadamu inakuwa si sawa ki afya. tabia hii ni kwamba ngiri watoto huwa wanakula Kinyesi cha mama yao mara kadhaa ktk kipindi hiki. Licha ya tabia hii kubeba sura ya kinyaa kwetu binadamu, hali hii ni muhimu sana kwa ngiri mtoto kwani ndio inayompa uwezo wa kupata lishe iliyomo ktk nyasi atakazokuwa anakula akiachana na maziwa.

Anapozaliwa, ngiri mtoto anakuwa na upungufu mkubwa wa bacteria ambao huwa anawahitaji ktk mfumo wake wa mmeng'enyo wake wa chakula (digestion system). Bacteria hawa ndio wanaohusika ktk mchakato wa kumeng'enya nyasi na kuweza kumpa ngiri virutubisho toka ktk shibe ya nyasi. kwa kula nanihii ya mama yake, Ngiri mtoto anakuwa na nafasi ya kuwapata bacteria hao anaowahitaji toka katika nanihii ya mama yake ambayo huwa wanakuwemo vya kutosha. [Ahsante ya picha kwa Tom wa Kimasafaris]

2 comments:

  1. Umenifungua macho kwa kunipa kitu kipya. Nilikuwa namuona ngiri kama mnyama ambae hana mpango, kumbe kuna jambo la kujifunza kuhusu maisha yake.
    Shukran mdau kwa kazi nzuri ya kututoa matongotongo wenyeji wako

    ReplyDelete
  2. Ebwana ndio....., hii ya Ngiri mtoto ni zaidi ya shule.

    ReplyDelete