Monday, July 26, 2010

Kura ya maoni - Malazi

Kura ya maoni iliyokuwa ikirindima kupitia blog ya TembeaTz imetoa mwelekeo wa kwamba wadau hupendelea zaidi kufikia katika sehemu za malazi ambazo zipo ndani ya hifadhi waliyoitembelea. Kura ya maoni hiyo ambayo iliongozwa na swali lisemalo "Ungependa kulala wapi endapo utaitembelea hifadhi uipendayo?" ulifikia tamati kwa ushindi kwenda kwa sehemu zilizopo ndani ya hifadhi kujinyakulia kura nyingi dhidi ya sehemu ambazo zipo nje ya hifadhi. Licha ya kwamba swali halikuuliza aina ya malazi lakini ni dhahiri ya kwamba wadau waliotoa maoni yao wanapenda kuwa karibu kabisa na wanyama pori na mazingira yao pindi wanapoamua kufanya safari ya kwenda porini. picha juu ni moja ya vyumba vya hoteli ya Serengeti Serena lodge. hii ipo ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Maramboi luxury tented camp; hii ipo katikati ya hifadhi za Tarangire na Manyara ktk eneo ambalo ni game controlled area.

Ndovu camp site, Selous game reserve. Hii ipo nje ya pori la akiba la Selous (mpakani mwa pori na eneo la kijiji)

Hii ni public campsite iliyopo ktk eneo la Behobeho ndani ya pori la akiba la selous.

No comments:

Post a Comment