Friday, July 9, 2010

Korongo la Joni, Ngorongoro crater

Ni eneo ambalo lipo ndani ya teritory ya pride moja ya Simba iliyopo shimoni (Ngorongoro crater). Ni sehemu moja ambayo madereva wengi huja kwa matumaini ya kuona sharubu. Wengi hufanikiwa kuwaona japo wakati mwingine wanaweza kuwa kwa mbali. Siku hii tuliwakuta wengi tena kwa karibu. japo mmoja wao alikuwa amekaa mbali kidogo na wenzinie. Umemuona ktk hiyo picha juu?

Kwa Jinsi alivyoweza kuji - camouflage (kutumia mazingira kujificha) unaweza ukamsogelea hadi kwa ukaribu bila ya wewe kugundua au kumuona. Wanyama hujifunza kutumia mazingira yao ili kufanikisha mawindo na shughuli zao za kimaisha ndani ya maeneo ya hifadhi.
[Picha - Maktaba ya TembeaTz]

1 comment:

  1. Je kuna simba wangapi kny picha hiyo hapo juu? mimi naona mmoja tu!
    Mdau Bradford

    ReplyDelete