Monday, June 7, 2010

Wa juu... Serengeti NP

Ktk mti huu kuna wajuu amejificha, unaweza kumuona???

Mkia wake ndio uliomwezesha guide wetu kumuona na kutuambia kuwa ni wa Juu (Chui). Ilikuwa ni mida ya jioni tukiwa njiani kurudi hoteli kupumzika ndio tulipokutana na huyu wa Juu. tulikuwa tumeshakata tamaa ya kuona wa juu siku hiyo. Jinsi wanavyoweza kujificha na kupotea ndio sababu inayofanya wasimamizi wa hifadhi kuweka sheria na taratibu ambazo mgeni unapashwa kuzifuata ili uweze kubaki salama. Wa juu hufanya mawindo yake mida ya usiku. Hutumia muda wake wa mchana kwa kupumzika na mara nyingi hupenda kupumzikia juu ya mti ambako anajua fisi na sharubu hawatamvamia au kumsumbua. Elewa ya kwamba bwana afya (fisi) ni mbabe wa wa juu. Endapo wa juu ataua mnyama na bwana afya akatokea (hata kama ni mmoja) basi wa juu huyo hatakuwa na budi ya kukimbia na kuwaachia jamaa windo lake ili kunusuru maisha yake. picha toka ktk maktaba ya TembeaTz, Serengeti NP

No comments:

Post a Comment