
Kufumba na kufungua huyu tumbili akawa tayari yupo juu ya roof ya gari yetu ambayo ilikuwa wazi akijaribu kuzama ndani kuangalia chochote. Kelele za kuhamaki kwetu zilimshtua na akaachana na hiyo biashara. Licha ya kwamba ni mdogo kiumbo lakini alikuwa na jeuri ya kumdhihaki mdau mfawidhi wa Tembea tz kwa sababu tu alikuwa ni mwanamke ambae alikuwa ndani ya gari muda wote. Mimi na Guide tulikuwa nje ya gari na mbali kidogo tukijinyoosha na kuagana na jamaa tukliokutana nao hapo picnic site ambao walikuwa wanafahamiana na guide wetu.
No comments:
Post a Comment