Thursday, June 24, 2010

Umbwe route

njia ya Umbwe ni moja ya njia ambazo zinaelezwa kuwa ni ngumu na zenye kuhitaji maandalizi ya kutosha. Ugumu wake unakuja kutokana na ukweli kwamba mpandaji anakuwa anapanda haraka hali ambayo haitoi muda wa kutosha kwa mwili wa mpandaji kuanza kujiandaa kwa changamoto za kimazingira. Kwa sababu hii, wengi (beginers) hupendelea zaidi Marangu route ambayo njia zake zinapanda (ascend) vizuri na kuupa mwili muda wa kutosha kuji-adjust.


Sifa moja kubwa ya hii njia ni kwamba ni njia fupi sana ya kufika Uhuru point iliyopo ktk kilele cha Kibo. Hili halina ubishi kwani hata ukiwa Kibosho (inapoanzia route ya Umbwe) kilele cha kibo kinaonekana kwa karibu mno kama nilivyobahatika kukinasa ktk mtundiko uliotangulia (mlima umeachia). Lakini ufupi huu unakuja kwa gharama ya kuhakikisha kuwa umeuandaa mwili wako ili kuweza kupambana na mwinuko mkali. inachukua takriban siku 3 au 4 kufika uhuru ukitumia njia Umbwe wakati route nyingine mpandaji hutumia siku 5-6 kufika Uhuru point. Unapoamua kwenda kuupanda mlima Kilimanjaro ni vyema ukaomba maelekezo na ushauri kuhusu njia utakayotumia kuupandia mlima huu. Kwa yule ambae atakuwa anapanda mlima kwa mara ya kwanza, ni vizuri kutumia Marangu route na baadae kuja kuzijaribu hizi nyingine.
Tangazo unaloliona ktk taswira za hapo juu zinalenga kuwapitisha wageni ktk mazingira tofauti tofauti ya mlima wakati wa kushuka. Wapandaji wanaotumia Umbwe, humalizia safari zao ktk gate la Mweka. Unaweza kubofya hapa ili kupata dondoo za njia nyingine za kupandia mlima Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment