Tuesday, June 22, 2010

hifadhi ya Taifa ya Tarangire

Baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro, Timu ya TembeaTz ilielekea hifadhi ya Taifa ya tarangire ili kuweza kupata mawili matatu toka huko. Tunamshukuru mungu ziara ya kikazi ndani ya hifadhi ya Tarangire imekuwa na mafanikio makubwa. Mengi tulioyaona huko yatawajia kupitia blog yenu muipendayo

Hivi sasa ni kipindi cha kiangazi ktk hifadhi ya Tarangire, na wanyawa ndio wanaanza kurudi ndani ya eneo la hifadhi. toka maeneo mbali mbali ambako huwa wanaenda kipindi cha masika kwa sababu mbalimbali.
Kwa sasa kikosi cha tembeaTz kimerejea Arusha mjini jana jioni na kuendelea na mapumziko mafupi baada ya ziara ambayo ilihusisha Game walking ya takriban saa moja ndani ya hifadhi.
Picha ni nyingi mno na kazi inayoendelea sasa ni uchambuzi wa picha sambamba na matukio na mambo tuliojifunza huko ili tuweze kukeletea ktk mtiririko utakaoleta maana kwako.

No comments:

Post a Comment