Moja ya sifa kubwa ya hifadhi ya taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara ni uwepo wa miti ya mibuyu kwa wingi sambamba na mibuyu hiyo kuwa mikubwa. Mibuyu ni mingi Tarangire, ukiwa ktk game drive hautamaliza kilometa moja bila kuuona mti wa mbuyu aidha kwa karibu au ukiwa mita chache toka ulipo. Jambo moja ambalo utalogundua (ukiwa mdadisi) utaona karibu mibuyu yote, ina mikwaruzo ya namna fulani ktk mashina yake kama vile kuna mtu alikuja kukata magamba ya mti kwa kisu au panga. Ktk mila na desturi za kiafrika ukataji huu wa magamba huenda sambamba na sababu za kitabibu ambapo magamba ya miti hutumika kama dawa. Ukweli ni kwamba, shughuli hii ya kuichuna mibuyu sio kazi ya mwanadamu bali ni kazi ya tembo ambao nao ni wengi ktk hifadhi ya Tarangire.
Mibuyu huhifadhi maji na unyevunyevu ktk shina lake. Tembo hukwangua mashina ya mibuyu ili kuweza kupata magamba ya mti huu ambayo huwa na majimaji yenye virutubisho na chumvichumvi ambazo tembo huzihitaji ktk ukuaji wake. baada ya kukwamgua kwa kutumia zile pembe zake, tembo hutafuna magamba hayo ili kuweza kupata majimaji yaliyomo ktk magamba hayo.
No comments:
Post a Comment