Friday, June 25, 2010

pozi hili ni hatari... mpitie mbali

Tukiwa ktk game drive ndani ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire tulimkuta huyu nyati akiwa amejificha ktk kichaka. Awali nyati huyu alikuwa sehemu ya wazi, alipotuona kwa mbali akakimbilia ktk hicho kichaka na kujificha kama umuonavyo ktk mtundiko huu. Alikuwa yuko peke yake eneo hilo

Nyati huishi ktk kundi na inapotokea mmoja wao akionyesha ukorofi au utovu wa nidhamu basi kundi humtenga na kumlazimu nyati huyo kuishi maisha ya upweke. Hali ya upweke huleta masononeko na mfadhaiko jambo ambalo humfanya nyati aliyetengwa kuwa mwenye hasira kali kwa kitu chochote kinachomkaribia. Pindi anapohisi hatari, nyati aliyetengwa hukimbilia ktk kichaka kwa lengo la kujificha na kufanya tathmini ya hatari au mvamizi wake kabla hajafanya shambulizi. na ndio hali aliyoionyesha nyati huyu tulipomkaribia kwa gari.

No comments:

Post a Comment