Thursday, June 3, 2010

Oliver's Camp, Tarangire

Oliver's Camp ni moja zilizomo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. Malazi ni kwenye tent kama unaloliona hapo juu. Ifikapo usiku kutembea ni lazima upewe escort ya ranger mwenye silaha unapokuwa unarudi chumbani (kwenye Hema) toka restaurant. Kwa kawaida, hotel au camp zinazojengwa ndani ya hifadhi hazina uzio. Hivyo unaweza amka asubuhi na kukuta sharubu au mnyama mwingine yeyote kaomba hifadhi mbele ya hema lako. Hiyo ni sehemu ya raha ya tented camping. Unaweza kupata dondoo zaidi kuhusu hii camp kwa Kubofya hapa . (Picha Mdau SB toka Antelope Safaris).

No comments:

Post a Comment