Thursday, June 3, 2010

Kibo Hut

Safari yetu ya taswira ya kuelekea kilele cha mlima Kilimanjaro inaendelea, safari hii tumefika point ijulikanayo kama Kibo Hut. Hapa ni baada ya kumaliza ile sehemu ijulikanayo kama the Saddle. Kibao cha ktk picha ya juu kinakuonyesha muda toka Kibo hadi kufika kituo kifuatacho cha Gilmans Point.

Taswira hii inakuonyesha japo kwa kuvizia, kilele cha kibo kinavyoonekana ukiwa Kibo hut.

Ofisi na nyumba za wafanyakazi wa KINAPA.

Kutokana na Kibo kuwa juu kutoka usawa wa bahari (mita 4700), vyumba vya kulala wageni huku vimejengwa kwa matofali tofauti na Mandara au Horombo ambako kumejengwa kwa mbao. Picha juu ni moja ya nyumba ambayo wapanda mlima huitumia kupumzikia wakiwa safarini.

Ma-chalii wenyewe sometimes huwa wanaangusha gari hata nje kwenye mahema madogo.

No comments:

Post a Comment