Wednesday, June 2, 2010

Tented camping; Tona Lodge

Hili lilikuwa ni kundi la wanafunzi toka Chuo kimoja huko nchini Marekani waliokuja Tanzania na kuamua kutembelea Milima ya huko Mbaga, Sama mkoani Kilimanjaro. Baadhi yao waliamua kulala kwenye mahema yao madogo ili kufurahia hali ya hewa na mandhari ya huko Milimani. Walifanya camping ktk eneo la Tona Lodge iliyopo huko huko milimani.


licha ya kujulikana kama ni hoteli, Tona Lodge inajishughulisha sana na utalii Asilia. Nia yao kuu ni kuwafanya wageni wanaoitembelea lodge hiyo kujua na kujifunza mila na desturi za jamii ya huko Milimani. Bofya hapa ili kupata dondoo zaidi kuhusu Tona Lodge na dhana nzima ya utalii asilia. Wasiliana nao ili kupata mpango mzima wa kwenda huko

No comments:

Post a Comment