Thursday, June 24, 2010

Game walking - Tarangire NP

Makubaliano ya awali ilikuwa Timu yote itashirikia ktk safari hii ya matembezi kwa miguu ndani ya Hifadhi. Lakini tulipofika getini hali ilibadilika na kujikuta nabaki peke yangu. Hii ilikuwa ni mara yangu ya 3 kufanya game walk baada ya ile ya Selous (2008) na nyingine niliyoifanyia Maramboi Camp siku moja kabla ya kufanya hii ndani ya Tarangire NP. Game walking ni namna nzuri ya mgeni kuweza kuona mambo mengi mengineyo ambayo ukiwa kwenye gari inakuwa vigumu kuyaona au hata kuyagusa na kujifunza zaidi. Safari yetu ilianzia geti kuu la Tarangire na tulitembea mpaka karibu kabisa na ilipo kambi ya Simba (Simba camp). Ilikuwa ngumu kujua umbali kwani njia ya kupita tuliamua wenyewe. Lakini safari nzima ilikuwa ni ya karibu saa moja na robo hivi. hatukufuata barabara ya kawaida. vituo vikiwa vingi injiani li kupata maelezo na elimu toka kwa Ranger niliyekuwa nae sambamba. Shukran sana kwa Ranger Majjid ambae ndie alikuwa ananisindikiza na kunielimisha. picha juu ni mimi nikiwa eneo ambalo tulikubaliana na wadau wengine watufuate na gari baada ya kuwapigia simu. Mitandao mikubwa ya simu inafanya kazi hivyo mawasiliano ya simu selula yanatumika kama kawa ndani ya hifadhi.

Tulikutana na makundi ya aina mbalimbali za Swala, pundamilia, Ngiri na kuona ndege wengi wa porini. Sehemu nyingine wanyama walikuwa wanakimbia lakini kundi hili lilisima na kutuwezesha kulisogelea kwa ukaribu zaidi.

Mara kadhaa nimewaona kobe lakini mara zote zimekuwa ni kwenye zoo au wikiwa ktk kifungo cha namna fulani. Safari hii nikiwa kwenye game walk na ranger tulimkuta huyu kobe mtoto akiwa nje ya moja ya mabwawa ya maji yaliyopo ndani ya hifadhi. bwawa hilo halifikiki kwa gari la wageni. ni kwa game walk pekee ndio unaweza kufika hapo. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo unakuwa huvioni unapokuwa unatembea hifadhini kwa gari.

Gari likija kutuchukua (Mimi na ranger) mahali tulipokubaliana kukutana. Unapofanya safari ya matembezi wengine hupenda kurudi getini (au pale mlipoanzia) na kisha kuendelea na ratiba nyingine- game drive. Siku hii tulikubaliana (na ranger) tutembee na kisha gari litufuate huko huko porini. kwa namna hii tuliweza kutembea umbali mrefu bila ya kuwa na wasiwasi wa muda na umbali wa safari ya kurudi getini. hapo ilikuwa ni mita kadhaa kabla ya kufika Simba Camp.

Mwanzoni, safari za matembezi huwa zinaleta uoga (siku ya kwanza) lakini ukishafanya moja na ukona elimu na uelewa unaoupata ufanyapo safari hizi, utajikuta kile uendapo porini au ktk eneo la hifadhi lenye wanyama pori utakuwa unataka kufanya game walk ili kupata fursa ya kujua zaidi. Nafasi unayoipata kuwa na ranger inakupa mwanya wa kuuliza na kupata maarifa mengi sana kuhusu wanyama wa porini na mazingira yao. pia unapata kuona changamoto ambazo hawa ranger wanakumbana nazo ktk jitahada zao za kulinda na kuhifadhi maeneo haya maridhawa. Kama unavyoona polisi wanavyofanya patrol mitaani, huko porini nako ranger huwa wanafanya patrol ktk maeneo mbalimbali. Wakati mwingine patrol zao hufanywa kwa miguu tena kwa umbali mrefu. TembeaTz inawapongeza wote wanajitoa mhanga ktk kulinda na kuhifadhi vivutio hivi ili viweze kuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na vifuatavyo.

No comments:

Post a Comment