Monday, June 7, 2010

Ni Mapitio ya wanyama wanaohama...

Alama unazoziona ktk maporomoko ya crater ni njia za wanyama ambao huwa wanahama toka Ngorongoro crater na kelekea ktk hifadhi ya Serengeti. Ingekuwa mjini unaweza ukasema ni mapito ya binadamu na vifaa vyao vya usafiri.
Wanyama nao wana mapito yao ambayo huyatumia wanapotoka sehemu moja kwenda nyingine. Mfumo huu una mazuri na mabaya yake. uzuri wake ni kwamba wanajiwekea mfumo mzuri wa navigation kati ya maeneo yao ya malisho na sehemu za kupata virutubisho vingine, maji n.k. Ubaya wake ni kwamba sharubu na ndugu zao nao sometimes huwa wanatega mitego yao ktk haya mapito ili kujipatia msosi. hii inatokana na uhakika wa kamba hapa ndio mapito yao yalipo.
Uwepo wa mapito haya ndio unaowawezesha hata wageni ambao huenda hifadhi ya Serengeti kuona Migration kujua wapi wakae ili kuwaona nyumbu na punda wanavyohama. Hufuata mapito hayo hayo mwaka nenda mwaka rudi. Picha hii imepigwa toka ktk balcony ya moja ya vyumba vya Ngorongoro Serena Lodge huko Ngorongoro crater.

No comments:

Post a Comment