Monday, June 7, 2010

Mijusi

Mjusi anaweza kuonekana kama ni mnyama ambae ni wa kawaida lakini ukweli ni kwamba ktk mchakato wa makuzi, mjusi anajikuza mwenyewe. Mjusi huzaliana kwa njia ya mayai. majike hutafuta sehemu muafaka ambayo ina usalama na kutaga mayai yake hapo. Baada ya shughuli ya Kutaga, mjusi jike hutoweka na anakuwa hana muda wowote na mayai yake hayo.

Mayai yale yakifikia muda wake, watoto hutoka (bila msaada) na kuingia duniani ki-vyao-vyao. ni Kawaida sana kukutana na mayai ya Mjusi kwenye kona za nyumba au samani lakini mama-mjusi anakuwa haonekani. wala usihangaike kumtafuta kwani kuna uwezekano mkubwa akawa hata hakumbuki ameyatagia wapi

Picha zote tatu ni Dodoma ktk nyakato tofauti tofauti.

No comments:

Post a Comment