Monday, June 21, 2010

mlima umeachia

Mwanzo niliposikia mmoja wa wenyeji wangu akisema "mlima umeachia", sikuelewa nini hasa kinaendelea. Punde si punde mwenyeji wangu mwingine ambae tuliambatana wote toka Dar alielewa nini maana ya kauli hiyo. Haraka haraka aliniambia nikamate kamera na tusogee mahali niupige picha mlima kwani kilele cha kibo 'Kimeachia', akimaanisha kuwa kinaonekana vyema. Nilipata kuelewa vyema lugha hii niliposogea sehemu ya wazi tuliyoweza kuipata kwa haraka na kisha kutizama upande ulipo Mlima na kujionea jinsi kilele cha Kibo ktk Mlima Kilimanjaro kilivyokuwa kikionekana vyema.

Picha hizi nilizipiga nikiwa Kibosho karibu kabisa na gate la kupandia mlima la Umbwe (Umbwe route). Kibosho ni muunganiko wa maneno ya Kibo na Show. Ni mahali ambapo kilele cha Kibo kinaonekana kwa karibu sana. Mara kadha nimewahi kuuona mlima Kilimanjaro, lakini safari hii nilipata bahati ya kuuona vyema tena kwa karibu mno nikiwa maeneo Kibosho. Muda si mrefu Kibosho kutakuwa na hotel/lodge/tented camp itakayokuwa inatoa huduma za malazi na chakula kwa wapanda mlima wanaopitia route ya Umbwe au kwa wale ambao watapenda kuachana na vurugu za mjini na kwenda kibosho kupumzisha akili huko milimani...

No comments:

Post a Comment