Ni kama utani lakini ndio ukweli wa mambo. Nilipokuwa Kibosho tulitembea Gate la Umbwe ambako ndio mwanzo wa Umbwe route. Tulipofika hapo tulikutana na huyu porter akianza safari yake ya kuelekea Uhuru peak. Wageni wake walikuwa wameshatangulia na wasindikizaji wengine.
Siku hii wasimamizi wa gate la Umbwe walinijulisha kuwa mpaka muda huo (ilikuwa ni kama saa 8 mchana hivi) tayari wageni wapatao 150 walikuwa wameshapanda Mlima kupitia gate hilo. Muda niliokaa hapo gateni nilipata bahati ya kuongea na wadau kadha na kupata dondoo mbali mbali kuhusu mchakato mzima wa kupanda mlima na route ya Umbwe pia. Utazipata hapa hapa, stay tuned..

No comments:
Post a Comment